Chuo Kikuu Rongo chafungwa baada ya ghasia kuzuka

  • | Citizen TV
    295 views

    Chuo kikuu Cha Rongo kimefungwa Kwa muda usiojulikana baada ya ghasia za wanafunzi kufuatia uchaguzi wa viongozi uliofanyika chuoni humo. Notisi iliyoandikwa na naibu chansela wa maswala ya wanafunzi Michael Mabururu ilidokeza kuwa Chuo kitasalia kufungwa kwa muda usiojulikana Kutokana na tofauti zilizozuka baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa. Kwa mujibu wa naibu chansela wa chuo hicho Samuel Gudu malalamishi ya baadhi ya wanafunzi waliogombea nyadhifa tofauti yaliwalazimu kuandaa mkutano wa dharura Ili kufunga Chuo hicho. ..