Citizen ilimtaja Anne Gikonyo miongoni mwa polisi walioachishwa kazi

  • | Citizen TV
    2,653 views

    Mtazamaji , kwenye taarifa zetu za nipashe za tarehe 21 Agosti , tulimtaja Anne Gikonyo kuwa miongoni mwa maafisa wa polisi walioachishwa kazi kwa madai ya kuwezesha washukiwa kutoroka kutoka seli za kituo cha polisi cha Gigiri hapa jijini Nairobi. Tumedhibitisha kuwa Anne Gikonyo hakuwa miongoni mwa maafisa wa polisi walioachishwa kazi kufuatia tukio hilo. Tunaomba radhi kwa Anne Gikonyo na athari zozote ambazo taarifa hiyo imemletea. kunradhi.