Daktari ambaye hutembea bila viatu katika maisha yake ya kila siku

  • | K24 Video
    123 views

    Kutembea bila viatu mara nyingi huhusishwa na umasikini katika jamii, lakini umewahi kufikiria kuwa kutembea pekupeku kunaweza kuwa na faida kiafya? Unapojiuliza swali hilo, kuna daktari mmoja kwa jina Hamisi Ali Kore ambaye kwa miaka miwili sasa ametembea bila viatu! si kenya tu bali pia ughaibuni. kwanini ameamua maisha hayo? Je mimi na wewe tunafaa kuiga?