Daktari anayedaiwa kuwaua wanawe afariki Nakuru

  • | Citizen TV
    Daktari James Gakara anayedaiwa kuwauwa wanawe wawili jumamosi wiki iliyopita ameaga dunia. Daktari Gakara ambaye alikuwa akipokea matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya rufaa ya Nakuru aliaga dunia leo asubuhi. Kufuatia kifo hicho huenda sasa kesi inayomkabili ikachukua mkondo tofauti kwani makachero wa DCI walikuwa wanasubiri daktari huyo kupata nafuu ili kupokea taarifa kamili kuhusu tukio la jumamosi. Afisa wa kitengo cha jinai katika eneo la Nakuru Magharibi Stephen Ambani anasema kuwa tayari watu wengine wameandikisha taarifa kuhusiana na kisa hicho. Kamanda wa Polisi Beatrice Kiraguri akisema kuwa huenda faili ya kesi hiyo ikafungwa