Daktari Denis Mukwege aeleza kilicho msukuma kugombea nafasi ya urais wa DRC

  • | VOA Swahili
    201 views
    Daktari Denis Mukwege aeleza kilicho msukuma kugombea nafasi ya urais DRC “Daktari Mukwege, wewe ni Mshindi wa Tuzo ya Nobel wa DRC, umetangaza unagombea urais wa DRC. Nini kilicho kusukuma kufanya hivyo?” “Nafikiri kitu cha kwanza kilicho nisukuma ni kwa miaka kadhaa wanajamii wa Congo wamekuwa siku zote wakiniuliza iwapo ninaweza kugombea urais wa Jamhuri hii. Hivyo basi, nilikuwa nikipata maombi, lakini hadi wakati huo, ilikuwa nahisi vigumu kuondoka katika eneo langu la uzoefu na kuanza kuingia katika njia hii mpya ya kuwasimamia watu wa Congo, na kuwasaidia. “Miaka kadhaa iliyopita, nimeshuhudia hali nchini kwetu – katika misingi ya usalama, siasa na jamii – imeharibika, kiasi kwamba hivi sasa tumekuwa katika hali ya kuwa na hofu, kwa hali ya uhai wetu, kwa umoja wa nchi yetu.” Kutokana na hali hii, nimejikuta katika mazingira ambayo ni lazima nitumikie wito huu, na leo, nimetoa jawabu la “ndiyo” kwa wito wa wanajamii wa Congo.” #DRC #RDC #Mukwege #Congo - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.