- 2,351 viewsDuration: 1:36Ni afueni kwa wakazi wa Langobaya na Baricho katika kaunti ya Kilifi baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa Daraja la Baricho Kwa kima Cha shilingi Bilioni 2.3. Kulingana na wakazi, eneo hilo limekuwa likishuhudia visa vya mara kwa mara vya watu kuvamiwa na wanyama wanapovuka mto huku wengine wakisombwa na Maji ya mto Galana. Kukamilika Kwa Daraja hilo Sasa kumewapa wakazi afueni kubwa kwani wataweza kusafirisha mizigo yao bila changamoto. Aidha wanafunzi wanaoelekea shuleni wataweza kuvuka daraja wakati wowote hata msimu wa mafuriko.