Daraja la Pai lililoporomoka Kajiado lajengwa

  • | Citizen TV
    2,065 views

    Kuporomoka kwa daraja la Pai kaunti ya Kajiado siku chache baada ya kuzinduliwa kulizua gumzo nchini huku Gavana Joseph Ole Lenku akilaumiwa kwa kuzindua daraja ambalo lilikuwa limengwa katika hali duni. Lakini sasa taswira ni tofauti huku daraja hilo sasa likiweza kustahimili mafuriko ya Mto Selenkei na kufanikisha usafiri hasa wakati huu wa mvua. Daraja hilo linaunganisha Kajiado Kusini, Kati na Mashariki. Daraja lililoporomoka liligharimu shilingi million 100.