Daraja refu zaidi duniani lafanyiwa majaribio

  • | BBC Swahili
    2,632 views
    Daraja la Huajiang Grand Canyon nchini China limefanyiwa majaribio ya siku tano kabla ya kufunguliwa rasmi mwishoni mwa Septemba. Jaribio la mzigo ndilo hatua ya mwisho kabla ya kuidhinishwa kwa matumizi ya magari. Timu ya majaribio iliendesha malori 96 na kuyaweka kwenye maeneo maalum ili kupima uimara wa muundo wa daraja hilo. Daraja hilo, ambalo linainuka kwa urefu wa mita 625 juu ya mto katika mkoa wa Guizhou, litakapokamilika litaweka rekodi ya kuwa daraja refu zaidi duniani na lenye upana mkubwa zaidi kuwahi kujengwa katika eneo la milimani. @frankmavura #bbcswahili #china #miundombinu Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw