DCI wamemkamata mshukiwa mkuu wa ujambazi Trans Nzoia

  • | Citizen TV
    730 views

    Maafisa wa upelelezi wa Jinai (DCI) katika Kaunti ya Trans Nzoia wamefanikiwa kumtia mbaroni mshukiwa mkuu anayedaiwa kuwa kiini cha msururu wa visa vya wizi vilivyoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo. Kamanda wa Polisi wa eneo la Trans Nzoia Magharibi, Erick Ng’etich, amesema kuwa operesheni hiyo ilifanikishwa baada ya msako mkali wa muda mrefu. Mshukiwa huyo, ambaye ni mkazi wa mtaa wa Tuwan, alipatikana akiwa na bunduki tano za kujitengenezea, risasi tano, misokoto 40 ya bangi, pamoja na vifaa vya kutengeneza pesa bandia vikiwemo kemikali, karatasi na mashine maalum ya kuchapisha. mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi huku uchunguzi ukiendelea kabla ya kufikishwa mahakamani.