Dhiki ya kina mama wachanga katika hospitali za Kajiado

  • | Citizen TV
    116 views

    Wasichana wadogo wanapata dhiki kujifungua katika baadhi ya hospitali za kaunti ya Kajiado wakilalamikia manyanyaso na kutelekezwa kwasababu ya umri wao mdogo.Ndio madhila waliyopitia wasichana wawili wenye umri wa miaka 14 na 15 baada ya kubeba mimba na kufikia wakatiw a kujifungua. Hali hiyo ilisababisha mmoja wa wasichana hao kumpoteza mwanawe punde tu baada ya kujifungua akidai kukosa huduma kwa wakati uliofaa