- 248 viewsDuration: 3:45Ongezeko la visa vya dhuluma za kijinsia miongoni mwa watoto pamoja na mimba za utotoni katika kaunti ya Busia limeibua wasiwasi mkubwa. Katika eneo la Teso Kaskazini idadi ya wasichana waja wazito ikipanda hadi asilimia 18 mbali na kuongezeka kwa maambukizi ya HIV miongoni mwa vijana. Sasa wadau kwa ushirikiano na idara ya afya ya kaunti ya Busia wamezindua kampeni maarufu ya Back to School ili kuhakikisha asilimia 100 ya wanafunzi wanarejea shuleni muhula huu.