DJ mashuhuri nchini akamatwa kwa kumpiga na kumua afisa wa polisi

  • | Citizen TV
    5,251 views

    Mcheza Santuri Mashuhuri Nchini Amekamatwa Akihusishwa Na Shambulio Dhidi Ya Afisa Wa Polisi Anayehudumu Katika Kaunti Ndogo Ya Dagoreti Ambaye Baadaye Alifariki Kutokana Na Majeraha. Mcheza Santuri Huyo Ambaye Kwa Sasa Anazuiliwa Katika Kituo Cha Polisi Cha Kabete Pamoja Na Mlinzi Wake, Dereva Na Mpiga Picha Anadaiwa Kumvamia Inspekta Felix Kelian Tarehe 16 Mwezi Huu. Afisa Huyo Kulingana Na Ripoti Ya Matibabu Alifariki Siku 6 Baadaye Akipokea Matibabu Katika Hospitali Ya Nairobi West.