DRC: Wachimba madini waliokwama wanusurika kufunikwa na kifusi

  • | VOA Swahili
    5,403 views
    Kanda ya video inawaonyesha wachimba madini tisa wa Congo bila ya kutarajiwa wakijitokeza kutoka katika kifusi cha machimbo ya dhahabu na kuserereka katika mteremko mkali huku mashuhuda wakipiga kelele za furaha ambazo zimevuma huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mwisho wa furaha ambao ni nadra kwa habari ya kawaida inayotokea kila siku. Ajali katika migodi ni nyingi katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ya Kati, hususan katika machimbo madogo madogo ya wachimbaji wa kawaida kama yale yaliyoko jimbo la Kivu Kusini yaliyoporomoka Jumamosi kufuatia mvua kubwa. Video hiyo inamuonyesha mtu mmoja akiwa hana kizuizi chochote pembeni ya mteremko mkali wa kifusi, akiharakisha kuchimba kwa koleo wakati kikundi cha watu wengine wakiwa wamesimama pembeni katika mduara mkubwa wakimzunguka, na kuangalia. Ghafla, mchimbaji ajitokeza kutoka katika kifusi, kama mtu anayepenya katika bomba, na kuserereka kuelekea chini, akisukumwa na juhudi yake, huku wanaoangalia wakifurahia kwa mshangao na furaha. Muokoaji huyo baada ya hapo anaonekana akiongeza juhudi mara dufu, akiacha koleo na kuendelea kutumia mikono yake kufukua. Mchimbaji mwingine mara anatokea, kisha mwingine, na ndani ya dakika mbili jumla ya wanaume tisa wametoka wakiwa hai na bila ya tatizo. Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters #DRC #RDC #Congo #gold #minerals #accidents - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.
    accident