Duale amuonya mmiliki wa Mediheal Swarup Mishra

  • | Citizen TV
    693 views

    Waziri wa Afya Aden Duale ametishia kumfurusha kutoka nchini mmiliki wa Hospitali ya Mediheal, Dkt. Swarup Mishra, kufuatia madai ya kuhusika katika sakata la ulanguzi wa figo. Akizungumza mjini Eldoret mapema leo, Duale alisema ananuia kutekeleza mapendekezo ya ripoti ya uchunguzi kuhusu biashara haramu ya figo na tayari ameiwasilisha bungeni. Aidha duale anadai kuwa baadhi ya waliotolewa figo wametoweka.