Duale aonya familia ya rais mstaafu isikaidi agizo la kusalimisha silaha

  • | Citizen TV
    16,874 views

    Waziri wa ulinzi Aden Duale leo ameonya kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya familia ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta iwapo hawatatii amri ya kusalimisha silaha anazodai wanamiliki kinyume na sheria. Duale akidai kuwa rais mstaafu amekuwa akihusika katika kufadhili maandamano ya kupinga serikali yanayoongozwa na Azimio la Umoja. Serfine Achieng Ouma anaarifu huku sasa ikibainika kuwa nyumba tatu zilizolengwa kwenye msako wa silaha ni za wanasiasa