Dunia yaomboleza kufuatia kifo cha gwiji wa soka kutoka Argentina Diego Maradona

  • | BBC Swahili
    Hujambo? karibu katika matangazo ya AMKA NA BBC;- Katika Amka Na BBC asubuhi hii... Viongozi mbalimbali wa kimataifa wamimina salam zao za rambirambi kufuatia kifo cha gwiji wa soka Diego Maradona, Argentina yatangaza siku mbili za maombolezo. Mshabiki katika jiji la Napoli nchini Italia alipocheza kwa muda mrefu nao wanaimba tungo za kumsifu.Lakini je alikuwa na haiba gani? Na katika gumzo leo hii tunangazia changamoto ya teknolojia katika kuzikuza ama kuzidumaza lugha za makabila utakuwa nami Regina Mziwanda na michezoni utakuwa na David Nkya #AMKANABBC #DiegoMaradona #Ethiopia