Dunia yaonywa kuchukua tahadhari kuhusu ongezeko la joto | VOA Swahili

  • | VOA Swahili
    119 views
    Shirika la hali ya hewa la umoja wa mataifa WMO lilitoa ripoti Jumatano inayoeleza kwamba joto limeongezeka kufikia viwango vya juu havijawahi kushuhudiwa na kuonya nchi za dunia kuchukua tahadhari ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ili kupunguza joto kali duniani. Wimbi la joto kali linakumba kwa wakati huu nchi za Afrika mashariki na Kati na nchi moja wapo Sudan kusini imeamuru shule zote kufungwa kwa wiki mbili kutokana na kuongezeka joto nchini humo. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.