EACC inamzuilia gavana wa Marsabit Mohammud Ali na aliyepita wa kaunti hiyo, Ukur Yattani

  • | Citizen TV
    1,928 views

    Gavana wa Marsabit Mahmoud Ali na Gavana aliyepita wa kaunti hiyo, Ukur Yattani wanazuiliwa na maafisa wa EACC baada ya kukamatwa mapema leo kwa madai ya ufujaji wa zaidi ya shilingi bilioni nane pesa za kaunti hiyo. Wawili hao pamoja na maafisa wakuu wa kaunti wanaendelea kuhojiwa na maafisa wa EACC mjini Marsabit na Nairobi kabla ya kufikishwa mahakamani.