EACC yatahadharisha serikali kuu na kaunti

  • | Citizen TV
    2,373 views

    Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini - EACC, imeonya serikali kuu na zile za kaunti dhidi ya kutumia janga la mvua ya el nino inayosubiriwa kuanza mwezi huu kufyonza pesa za umma. Afisa mkuu wa tume hiyo Twalib Mbarak amewataka maafisa wanaohusika na uhasibu kuhakikisha kuwa wamefuata taratibu za kutoa kandarasi akisema kuwa watawajibika binafsi endapo pesa za umma zitafujwa. Haya yanajiri huku serikali ya kaunti ya Nairobi ikikaza kamba ili kujiandaa kukabiliana na athari za mvua hiyo