Skip to main content
Skip to main content

EACC yatwaa mali ya shilingi milioni 207 kutoka kwa afisa wa zamani wa kaunti ya Trans Nzoia

  • | KBC Video
    378 views
    Duration: 2:46
    Tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi nchini EACC imefanikiwa kurejesha mali ya thamani ya zaidi ya shilingi Milioni-207 kutoka kwa afisa mmoja wa zamani wa serikali ya kaunti ya Trans Nzoia. Tume hiyo ilipata maagizo ya mahakama ya kutwaa mali hiyo ya thamani kubwa iliyo katika maeneo ya Mombasa na Bungoma, pamoja na magari ya kifahari yanayomilikiwa na Andrew Biketi Musuya, aliyekuwa mhasibu katika wizara ya Afya ya Umma na Usafi, na serikali ya kaunti ya Trans Nzoia. Musuya alishindwa kueleza chanzo cha utajiri wake ambao unadaiwa kupatikana kwa njia zisizo halali. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive