EACC yazuia ununuzi wa majumba mawili Nairobi

  • | Citizen TV
    2,227 views

    Tume ya kupambana an ufisadi nchini - EACC imepata idhini ya kuzuia ununuzi wa majumba mawili ya kifahari yaliyoko jijini Nairobi, kwa madai kuwa yalinunuliwa kiharamu na fedha za umma. Watu 13 akiwemo aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ununuzi katika serikali ya kaunti ya Vihiga Nathaniel Ahaza pamoja na mkewe, wanashutumiwa kwa kukiuka sheria za ununuzi na ubadhirifu wa kima cha shilingi milioni kumi na tatu kati ya mwaka wa 2014 na 2015.