Ebwali Boys ndio mabingwa wa Chapa Dimba na Safaricom kanda ya Magharibi

  • | Citizen TV
    381 views

    Ebwali Boys ndio Mabingwa wa Safaricom chapa dimba ukanda wa magharibi baada ya kuwalaza compel sportif bao moja bila jibu. Mshambulizi nyota wa sportif alipoteza penalti ambayo ingesawazisha mambo katika uga wa Bukhungu. Kina dada wa Brenda ndio mabingwa wa magharibi upande wa kina dada baada ya kuwalaza lugari sportif mabao mawili kwa moja... Brenda girls na Ebwali Boys watawakilisha ukanda wa magharibi katika fainali za kitaifa zitakazoandaliwa mwakani. Washindi wametia kibindoni laki mbili unusu huku waliomaliza nafasi ya pili compel sportif na lugari progressive wakipata laki moja unusu kila timu. Kipute hicho sasa kinaelekea Kisumu kwa fainali za ukanda wa Nyanza mwezi ujao.