Aliyekuwa Waziri wa Habari na Teknolojia, Eliud Owalo, amezindua chama cha kisiasa kitakachobeba azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Owalo amesema chama chake cha Peoples Prosperity Party (PPP) kitajikita katika kuimarisha uchumi wa taifa, kufanya mageuzi ya ushuru, kukuza ustawi wa michezo na kuhakikisha utekelezaji wa Katiba.
Aidha, amesema serikali zilizopita zimeshindwa kushughulikia ipasavyo changamoto zinazowakabili Wakenya na kwamba chama chake kinatoa mbadala wa uongozi.