Eneo bunge la Juja lapata zaidi ya shilingi milioni 80 kupitia NG-CDF

  • | Citizen TV
    144 views

    Eneo bunge la Juja limetengewa zaidi ya shingi milioni 80 kupitia hazina ya serikali ya ustawi wa maeneo bunge ili kujenga madarasa mapya, kukarabati madarasa yaliyokuwa yamechakaa, na kujenga maabara katika eneo la Juja, kaunti ya Kiambu. Uboreshaji wa shule hizo katika eneo bunge hilo unakusudiwa kuimarisha matokeo ya wanafunzi katika shule zote na pia kuboresha miundombinu.