Eneo la Baragoi kaunti ya Samburu lapata taswira mpya

  • | Citizen TV
    854 views

    Eneo la Baragoi kaunti ya Samburu kwa miaka mingi lilishuhudia misukosuko ya usalama na uvamizi uliosababisha mauaji na makovu kwa wakaazi walioishi eneo hili. Taarifa za mauwaji, mazishi na hata majeraha zilikuwa nyingine kwa zaidi ya miongo mitatu ila sasa sura inaonekana kubadilika. Juhudi za miaka miwili za amani zikichora picha mpya ya eneo hili la Baragoi, ambako mwanahabari wetu Bonface Barasa ametuandalia taarifa ifuatayo