EU yatahadharisha shambulizi Rafah litaleta janga kwa wakimbizi

  • | VOA Swahili
    439 views
    Moshi ukitanda katika anga ya Gaza kama unavyoonekana Jumatatu (Februari 19) kutoka mahema ya kambi ya Rafah ya Wapalestina waliokoseshwa makazi. Umoja wa Ulaya Jumatatu uliitahadharisha Israel isianzishe mashambulizi huko Rafah ambako mawaziri walisema italeta janga kwa wakimbizi takriban milioni 1.5 waliojazana katika mji huo ulioko kusini kando ya Gaza. Israel inajitayarisha kufanya uvamizi wa ardhini katika eneo finyu la kusini mwa mji, ambao imeuita ni ngome ya mwisho inayodhibitiwa na Hamas baada ya takriban miezi mitano ya mapigano. Israel inatarajia kuendelea na operesheni kamili ya kijeshi huko Gaza kwa wiki nyingine sita hadi nane wakati ikijitayarisha kuivamia Rafah, maafisa wanne wanaoufahamu mkakati huo wamesema. Wakuu wa Jeshi wanaamini wanaweza kuharibu vikali uwezo wa kijeshi uliosalia wa Hamas kwa kipindi hicho, ikitoa njia kuhamia katika awamu ya mashambulizi ya malengo ya nguvu ya chini na operesheni ya majeshi maalum, kulingana na maafisa wawili wa Israeli na maafisa wa ukanda wakiomba kutotajwa majina yao ili waweze kuwa huru kuongea. Kuna nafasi ndogo sana ya Serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu itazingatia ukosoaji wa kimataifa kusitisha mashambulizi ya ardhini huko Rafah, alisema Avi Melamed, afisa wa zamani wa intelijensia wa Israeli na msuluhishi katika Intifada ya kwanza na ya pili, machafuko, ya mwaka 1980 na 2000. Takriban Wapalestina 29,092 wameuawa na wengine 69,028 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi ya anga katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7, wizara ya afya Gaza ilisema Jumatatu. Katika kipindi cha saa 24, Wapalestina 107 waliuawa na wengine 145 walijeruhiwa, wizara hiyo iliongeza katika taarifa yake. -Reuters ⁣⁣ #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #iran