Familia mbili zinalilia haki baada ya wenzao kuuawa

  • | K24 Video
    63 views

    Familia mbili katika kijiji cha Gitiri eneo bunge la Kiharu zinalilia haki baada ya Mary Njoko ajuza wa miaka 75 na mwenzake Jane Wambui wa miaka 85 kupigwa na kuteketezwa hadi kufa kwa tuhuma za kujihusisha na ushirikina. Kulingana na familia hizo, wazee hao hawajihusishi na uchawi kama inavyodaiwa na wanataka haki itendeke kwa waliohusika na mauaji ya wakongwe hao