Familia moja Kitui inaitaka serikali iwasaidie kutafuta jamaa zao walioenda Shakahola

  • | K24 Video
    37 views

    Wakati huohuo familia moja katika kaunti ya Kitui inaitaka serikali iingilie kati na kuwasaidia kuwapata jamaa zao baada ya kuwatafuta kwa muda sasa bila ya kufua dafu. Baba wa familia hiyo inayoishi katyethoka anahofia kuwa mabinti wake wawili pamoja na wana wao wanne ni miongoni mwa wafuasi wa paul mackenzie waliopoteza maisha katika msitu wa Shakahola, kaunti ya Kilifi.