Familia moja mtaani Westlands afurushwa kutoka nyumbani kwao

  • | Citizen TV
    850 views

    Familia moja mtaani Westlands inalilia haki baada ya kufurushwa kutoka makao yao ya miaka 46 na nyumba yao kubomolewa kufuatia mzozo wa ardhi. Familia hiyo ililetewa stakabadhi za mahakama na mwekezaji mmoja aliyedai kununua ardhi hiyo mwaka wa 2010 siku ya ijumaa. Aliyewaletea stakabadhi hiyo alikuwa ameandamana na kundi la vijana walio wahamisha kwa lazima na baadhi yao kuiba mali. Nyumba hiyo ilibomolewa wikendi hii na hadi wakati tulipozuru eneo hilo, vijana wanaoaminika kutumwa na mwekezaji huyo walikuwa wanakusanya vifaa vilivyobaki kwenye vifusi. Polisi wanasema mwekezaji huyo hakufuata sheria na hatua zitachukuliwa dhidi yake.