Familia tatu zinazozania ardhi mtaani lavington

  • | Citizen TV
    2,029 views

    Idara ya mahakama imetoa taarifa kuhusiana na utata wa ardhi katika mtaa wa kifahari wa Lavington, Nairobi unaohusisha familia tatu. Mahakama imedhibitisha kuwepo kwa kesi hiyo ambayo walalamishi wanadai umiliki wa ardhi hiyo ya ekari moja kwa sababu ya kuishi hapo kwa miaka 27 wakidai mmiliki aliyeingia ndani ya eneo hilo jumamosi wiki jana hajaonekana hapo kwa miaka hiyo yote. Mahakama hata hivyo imesema haitajatoa agizo lolote kuhusiana na suala hilo huku kesi hiyo ikitarajiwa kuskizwa tarehe 18 mwezi Septemba.