Familia ya kijana aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo la Mwiki, Kasarani yadai haki

  • | Citizen TV
    2,424 views

    Huzuni na hasira zimetanda eneo la mwiki, Nairobi baada ya kijana wa miaka 19 kupigwa risasi na kuuawa Ijumaa jioni. Wakaazi wanadai alipigwa risasi na afisa wa polisi wakati wa maandamano ya kutafuta haki kwa Abigael Wanjiku, msichana wa miaka 18 aliyebakwa na kuuawa Alhamisi. Joshua Steven, alifyatuliwa risasi akiwa anatoroka vitoa machozi. Familia yake imesalia na majonzi, huku wakazi wakiandamana kutaka haki itendeke.