Familia yadai haki kufuatia mauaji ya jamaa yao Ugunja

  • | Citizen TV
    516 views

    Familia moja kutoka kutoka eneo la Ugunja inalilia haki kufuatia mauaji ya jamaa yao. Inadaiwa kuwa Gabriel Waeke ambaye alikuwa mwashi kutoka kwenye kijiji cha Imbaya alipigwa hadi kufa baada ya kuuza toroli ya jirani yao. Kakake mwendazake Stephen Ogutu anadai kuwa Gabriel alichukuliwa na jirani yao mmoja aliyempiga kwa silaha butu kisha kumuacha kwenye hali mahututi. Ogutu akisema kuwa juhudi za kumkimbiza nduguye hadi katika hospitali ya kaunti ndogo ya Ambira hazikufua dafu kwani alifariki alipokuwa akipokea matibabu. Sasa wanataka uchunguzi wa haraka kufanywa na wahusika kuchukuliwa hatua