Familia yadhamiria kumuoza mtoto wa miaka 9 Turkana

  • | Citizen TV
    1,479 views

    Huku Serikali inapojizatiti kutoa elimu ya msingi ya bure na kwa wote humu nchini, imebainika kuwa asilimia kubwa ya watoto wasichana katika sehemu za mashinani kaunti ya Turkana hawajajiunga na shule badala yake wanafichwa nyumbani na mwishowe kuozwa. Cheboit Emmanuel anasimulia kisa cha msichana mmoja mwenye umri wa miaka tisa kutoka kijiji cha Lorus ambaye licha ya umri wake mchanga amevikwa pete na kuozwa.