Familia yaomboleza vifo vya jamaa walioaga salama katika ajali, Nakuru

  • | Citizen TV
    1,902 views

    Familia moja katika eneo la Pipeline jijini Nakuru inaomboleza vifo vya jamaa wao sita walioaga dunia kwenye ajali ya barabarani eneo la Salama kaunti ya Makueni jumatatu usiku. Familia ya Joseph Macharia ilipoteza ndugu,watoto wanne na mama kwenye ajali hiyo. Jamaa hawa walikuwa miongoni mwa watu 14 walioabiri gari la abiria la Spanish lililogongana ana kwa ana na trela.