- 1,515 viewsDuration: 1:53Imekuwa ni afueni kubwa na faraja kwa familia moja katika kijiji cha Katanin, Kaunti ya Nandi, baada ya kupokea fidia kutoka kwa Shirika la huduma kwa Wanyamapori (KWS) ya kifo cha mwana wao kilichotokea miaka kumi iliyopita baada ya kuumwa na nyoka. Akizungumza wakati wa hafla ya kutoa fidia hiyo, Katibu wa Uhifadhi katika Idara ya Wanyamapori, Dkt. John Chumo, alisema kuwa serikali inatumia karibu shilingi bilioni moja kila mwaka kufidia wananchi kutokana na vifo, majeraha, au uharibifu wa mali unaosababishwa na wanyamapori .