Familia za vijana wanne waliopotea Mlolongo Disemba mwaka jana wanalilia haki

  • | K24 Video
    144 views

    Familia za vijana wanne waliopotea Mlolongo Disemba mwaka jana wanalilia haki kwa serikali baada ya wawili kati yao kupatikana mwezi moja baadaye katika chumba cha maiti cha city. Wakizungumza hii leo, wakili Dan Maanzo na mwanaharakati Hussein Khalif wanamtaka Rais William Ruto, idara ya polisi na waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen watoe maelezo ya wanaotekeleza utekaji nyara ilhali wanasimamia usalama wa nchi. Inashukiwa kuwa miili ya Stephen Mbisi na Karani Muema pia imehifadhiwa katika makafani ya city.