- 624 viewsFamilia za waathiriwa wa maandamano ya Jumatatu ya kupinga bei ya juu ya mafuta zinaendelea kuomboleza vifo vya ghafla vya wapendwa wao. Huko Naivasha, Kaunti ya Nakuru, familia ya kijana wa miaka 17 inalilia haki baada ya kijana huyo kupigwa risasi na maafisa wa usalama alipokuwa akielekea nyumbani kutoka kazini. Wanaharakati sasa wanataka ukatili na mauaji yanayoripotiwa katika maandamano kusitishwa na kuchunguzwa kwa kina.