Skip to main content
Skip to main content

Familia za waathiriwa wa mkasa wa mgodi Kapsabet zinadai haki inacheleweshwa miaka 3 baadaye

  • | Citizen TV
    148 views
    Duration: 1:54
    Familia za waathiriwa wa mlipuko uliotokea katika mgodi wa dhahabu wa Karebe mwaka 2023 walifika katika Mahakama ya Kapsabet wakitaka haki kwa jamaa zao waliopoteza maisha katika tukio hilo. Jamaa hao walikusanyika nje ya mahakama wakiwa wamebeba mabango wakitoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa waathiriwa. Mlipuko huo ulisababisha vifo vya watu watatu na kuwaacha wengine na majeraha mabaya, huku familia zilizoathirika zikisema kuwa bado hazijapata majibu ya kuridhisha kuhusu kilichosababisha tukio hilo. Kesi hiyo iliyokuwa inapasa kusikizwa siku ya Jumatatu katika Mahakama ya Kapsabet hata hivyo iliahirishwa hadi tarehe 26 Mei. Wakizungumza nje ya mahakama, mawakili wa familia za waathiriwa walisema kuwa kucheleweshwa kwa kesi hiyo kumeongeza machungu kwa familia ambazo zimekuwa zikisubiri haki kwa muda mrefu.