Familia zaandamana wakiitaka serikali kufanikisha malipo ya mashamba yao Nyeri

  • | K24 Video
    116 views

    Polisi huko Kiriti Kangocho kaunti ya Nyeri wamelazimika kutumia vitoa machozi kuzitawanya familia 30 zilizokuwa zimeandamana wakiitaka serikali kufanikisha malipo ya mashamba yao,yalioathirika na ujenzi wa barabara ya kutoka Kenol kuelekea marua. Familia hizi zimeteta kuwa tangu kuanzishwa kwa ujenzi wa barabara hii miaka mitatu iliyopita, juhudi zao za kuitaka tume ya ardhi kuwafidia zimekuwa zikigonga mwamba.