Familia zaanza kupokezwa miili ya wapendwao waliouwawa kwenye msitu wa Shakahola

  • | Citizen TV
    1,398 views

    Serikali imeipokeza familia moja miili ya wapendwa wao wanne waliouwawa kwenye msitu wa Shakahola huku shughuli ya kukabidhi familia maiti za jamaa zao zikianza leo. Familia ambazo ziliwasilisha chembechembe za DNA ili kuambatanishwa na maiti iliyofukuliwa zitaendelea kuchukua miili iliyotambuliwa Jumatano na Alhamisi.