- 172 viewsDuration: 1:49Familia zaidi ya 800 katika eneo bunge la Kipkelion Mashariki, Kaunti ya Kericho, zinatarajiwa kunufaika na mpango wa serikali wa kuunganisha umeme, hatua inayolenga kuboresha maisha ya wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi mashinani. Mradi huo ni sehemu ya mpango mpana wa serikali ya kitaifa wa Last Mile Connectivity, ambapo jumla ya Shilingi bilioni 1.5 za kusambaza umeme katika Kaunti ya Kericho zimetengwa.