Skip to main content
Skip to main content

Familia zaomba serikali iwarejeshe wakenya wanane waliofungwa Libya

  • | Citizen TV
    950 views
    Duration: 3:30
    Usiku wa leo, familia za Wakenya wanane waliokwama nchini Libya zimeiomba serikali kuingilia kati na kuwasaidia kuwarejesha nyumbani. Watu hao, ambao walielekea Libya kutafuta ajira, kwa sasa wanasemekana kuwa gerezani mjini Benghazi. Kumekuwa na madai kuwa kile kilichoanza kama ahadi ya ajira kimegeuka kuwa kesi za ulanguzi wa binadamu, kutolipwa mishahara, na hatimaye kufungwa gerezani. Mwanahabari Odee Francis amezungumza na Wakenya walioko Libya pamoja na familia za waathiriwa, na kuandaa taarifa hiyo.