Naibu Kamishna wa Keiyo South, Michael Odulwo, ametoa wito kwa wakazi wanaoishi katika maeneo yaliyoko kwenye hatari ya maporomoko ya ardhi kuhama mara moja ili kuepuka maafa.
Akizungumza wakati wa tathmini iliyokuwa ikifanyika katika vijiji vya Kipkaa, Siroch, na kando ya barabara kuu ya Iten kuelekea Kabarnet, Odulwo amesema kuwa Maafisa wa usalama, pamoja na wa shirika la Msalaba Mwekundu wanaendelea kuzuru maeneo kadhaa ili kutathmini hatari ya maporomoko. Takriban familia nane zimeachwa bila makao baada ya nyumba zao kuharibiwa, huku mifugo wakipotea kufuatia maporomoko hayo yaliyotokea siku chache zilizopita.Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa familia zilizoathirika zinahitaji msaada wa dharura.