Familia zinawatafuta jamaa zao waliosombwa na maji, Nairobi

  • | Citizen TV
    1,191 views

    Idara ya Utabiri wa hali ya anga sasa imetabiri mvua kubwa na mafuriko katika baadhi ya maeneo ikiwemo Nairobi, maeneo ya kati na Pwani. Utabiri huu ukijiri zaidi ya majuma mawili baada ya mvua kubwa iliyoshuhudiwa Nairobi kusababisha vifo vya watu 11 na uharibifu wa mali. Hata hivyo, baadhi ya familia bado zinatafuta miili ya jamaa zao waliosombwa na mafuriko hayo juma lililopita.