Skip to main content
Skip to main content

Familia zinazoishi karibu na mto Tana zimeanza kuhama

  • | Citizen TV
    762 views
    Duration: 1:37
    Familia zinazoishi karibu na mto Tana viungani mwa mji wa Garissa zimeanza kuhama baada ya mto Tana kuvunja kingo zake kutokana na kuongeza kwa viwango vya maji. Familia hizo zinasema kuwa japo zimeitikia wito wa serikali na idara ya utabiri wa hali ya hewa wa kuwataka kuondoka, hazina mahali mbadala pa kwenda. Waathiriwa hao sasa wanahofia kukubwa na njaa kutokana na uhaba wa chakula. Aidha wanaishi kwa hofu kuwa watoto wao huenda wakapata magonjwa kutokana na hali duni ya mazingira kwenye kambi za muda.