Fedha za Ustawi wa barabara

  • | Citizen TV
    227 views

    Kamati ya seneti kuhusu miswada imependekeza kuundwa kwa kamati ya uwiano ili kutatua utata wa fedha za ustawi wa barabara nchini. Wakiongea huko mombasa baada ya kuzuru Bunge la kaunti ya Mombasa maseneta hao wanataka serikali kuu kuwasilisha fedha za kaunti kwa muda unaofaa ili kufanikisha maendeleo. Spika wa kaunti ya mombasa Aharub Kharti ametaka fedha za umma kutumiwa jinsi ilivyopangwa ili kuwanufaisha wakenya.