'Filamu za mapigano zilivyonipa ujasiri’

  • | BBC Swahili
    Imekuwa ni nadra kwa wanawake kukishiriki katika michezo ya kupigana na hata katika filamu za mapigano. Sababu kuu ilimfanya Agnes kuingia katika mapigano ilikuwa ni manyanyaso waliyokuwa wakifanyiwa rafiki zake wa karibu hivyo kumpa nguvu ya kujifunza ili siku moja aweze kuwa mtetezi wao. Sasa wengi humuogopa wanavyomuona akipigana katika video mitandaoni na kuhisi ni uhalisia wa maisha yake huku akiwa na ndoto za kufungua darasa kwaajili ya kufundisha wanawake wenzie kupigana na kujihami endapo watakutana na manyanyaso kwa wanaume zao au jamii inayowazunguka. @BBC News Swahili #tanzania #wanawake #hakizawanawake