Fulu Miziki: 'Tunataka kuitunza Afrika'

  • | BBC Swahili
    341 views
    Huko Kinshasa, DRC, kikundi cha marafiki wameunda kundi la muziki ambalo ni rafiki wa mazingira liitwalo Fulu Miziki, ambalo lina maana ya 'muziki kutoka kwenye mapipa ya takataka' kwa Kilingala. Bendi imejipa dhamira kukusanya taka duniani kote na kuzigeuza kuwa vyombo vya muziki na mavazi, ili kuzuia Afrika kuwa dampo la taka duniani. #bbcswahili #muziki #congo