Fulusi za Mahasla: Hali ya sintofahamu yaendelea kutanda kuhusu utekelezaji wa Hustler Fund

  • | KTN News
    3,035 views

    Huku zikiwa zimesalia saa za kuhesabu kabla ya uzinduzi wa hazina ya hasla almaarufu hustler fund, mjadala mkubwa umesheheni kwenye mitadao ya kijamii kuhusu utekelezaji wake. Hali ya sintofahamu haswa miongoni mwa wananchi almaarufu mahasla wanaomezea mate hazina hiyo imeendelea kutanda, wengi wakijiuliza ni vipi wataweza kunufaika. Mwanahabari David Muthoka anaangazia kwa kina hazina hiyo itakayozinduliwa mwishoni mwa mwezi huu, na kujibu maswali nyeti ambayo yamekuwa yakiulizwa na mahasla kwenye mitandao ya kijamii, vibaruani na hata mitaani.