Gachagua ahimiza kanisa lishirikiane na serikali kukabili mihadarati

  • | KBC Video
    40 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua ametoa changamoto kwa makanisa kuungana na serikali kwenye vita dhidi ya pombe haramu na matumizi ya dawa za kulevya. Gachagua ambaye alikuwa akizungumza katika kaunti ya Nakuru wakati wa hafla ya kumtawaza askofu mpya, ilioandaliwa na kanisa la Kiangilikana nchini , alijiepusha na mjadala kuhusu siasa za eneo la Mlima Kenya. Hata hivyo, mkosoaji wake katika bunge la kitaifa Kimani Ichungwah akiongea katika eneo la Mathira, kaunti ya Nyeri , alikosoa pendekezo la Gachagua kuhusu ugavi wa rasli-mali za taifa, akisema pendekezo hilo linaweza kusababisha mgawanyiko.Maelezo zaidi ni katika taarifa yake Giverson Maina .

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News